Kufungua mlango wa usajili wa kushiriki kwenye semina ya hukumu za usomaji wa Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza ufunguzi wa semina ya hukumu za usomaji wa Qur’ani itakayo fanywa siku mbili kwa wiki chini ya ukufunzi wa Sayyid Dhulfiqaar Saburi.

Usajili unafanywa kwa njia ya mtandao au katika ofisi za Maahadi zilizopo Najafu/ Hannaanah/ barabara ya Posta.

Semina itakua na masomo mengi, miongoni mwa masomo hayo ni Hukumu za usomaji wa Qur’ani tukufu, kuanzia matamshi ya herufi, sifa za herufi na hukumu zake.

Nayo ni moja kati ya semina nyingi zinazofanywa na tawi la Maahadi, kwa lengo la kuongeza kiwango cha uwezo wa wasomaji, katika usomaji wa Qur’ani sahihi kwa kuzingatia hukumu za tajwidi.

Kumbuka kuwa semina zinazofanywa na Maahadi ya Qur’ani tukufu ni sehemu ya harakati muhimu, uongozi wa Maahadi unatoa kipaombele zaidi katika semina za Qur’ani kutokana na muitikio mkubwa wa watu pamoja na faida inayo patikana kwenye semina hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: