Kukutana kwa baraka ya Mtume wa Rehema -s.a.w.w- na bibi Khadija mwezi kumi Rabiul-Awwal

Maoni katika picha
Riwaya zinaonyesha kuwa mwaka wa ishirini na nane kabla ya Mtume kuhama Maka, Mtume (s.a.w.w) alimuoa bi Khadija bint Khuwailid (a.s), hatua tukufu na tukio muhimu katika historia ya uislamu, ndoa hiyo pamoja na kuwa tukufu pia ni tukio la pekee katika uislamu lililosaidia kuimarisha na kulinda uislamu.

Bibi Khadija (a.s) alikua mwanamke bora, tajiri, mzuri, alipewa jina la (Twahira) na jina la (bibi wa Makuraishi), watu wake walikua karibu nae sana.

Viongozi wa Makuraishi waliomba kumuoa, na wakamuahidi mali nyingi, lakini aliwakataa wote, akachagua kuolewa na Mtume (s.a.w.w) kutokana na tabia njema ya Mtume na utukufu wake, kuna dalili nyingi zinazo onyesha kuwa alikua sio mshirikina kama watu wa Maka, bali alikua ni muumini wa Dini ya Nabii Ibrahim (a.s).

Abuu Twalibu pamoja na ndugu zake na baadhi ya Makuraishi walienda kwa walii wake, Ammi yake Amru bun Asadi kwani baba yake alikua amesha uawa katika vita, wakamposa.

Historia inasema kuwa mwanamke wa kwanza kumuamini Mtume (s.a.w.w) ni mke wake Khadija bint Khuwailid, riwaya ya Ibun Abbasi inasema: “Hakika mtu wa kwanza kumuamini (s.a.w.w) ni Ali bun Abu Twalib (a.s) na mke wake Khadija bint Khuwailid”.

Bi Khadija alikuwa na heshima maalum mbele ya Mtume (s.a.w.w), Maisha yote Mtume (s.a.w.w) aliendelea kumtaja kwa heri na kusisitiza nafasi yake katika moyo wake, alikua anamsifu wala hakuna yeyote wa mfano wake, bibi Khadija (a.s) alikua ngome na msaada mkubwa kwa Mtume (s.a.w.w) katika wakati mgumu, alitoa mali zake zote kwa ajili ya Uislamu, ndoa hii tukufu ilijengwa katika misingi ya ubinaadamu, maadili mema, ukweli na uaminifu.

Ndoa hiyo ilikua na matunda mazuri, watoto wote wa Mtume (s.a.w.w) wanatokana na bibi Khadija (a.s), ispokua Ibrahim aliyezaliwa ni bi (Mariya Qibtiyya), watoto wa bi Khadija (a.s) ni: Qassim na Twayyib, walikufa Mtume akiwa Maka wakiwa wadogo, na Zainabu, Ummu-Kulthum, Ruqayya na Fatuma Zaharaa (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: