Hafla ya wanawake katika kusherehekea kuvishwa taji Imamu Mahadi (a.f)

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa hafla kubwa ya wanawake katika kumbukumbu ya kuvishwa jati Imamu Mahadi (a.f), aliyechukua majukumu ya uimamu akiwa na miaka mitano baada ya kifo cha baba yake Imamu Hassan Askariy (a.s), nayo ni siku ya kwanza ya Uimamu na uongozi wa muokozi wa binaadamu, na hoja ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, kwa lengo la kukuza utamaduni wa Mahadawiyya na kuonyesha mshikamano wa pamoja na Imamu wa zama.

Hafla hiyo imefanywa ndani ya sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) katika haram takatifu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhudhuriwa na mazuwaru wengi waliojaa furaha, kama sehemu ya kufanyia kazi kauli ya Imamu Swadiq (a.s) isemayo: (Mwenyezi Mungu awarehemu wafuasi wetu wameumbwa kutokana na mabaki ya udongo wetu na wametiwa maji ya uongozi wetu, wanahuzunika kwa huzuni zetu na wanafurahi kwa furaha zetu).

Makamo kiongozi wa idara bibi Taghridi Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kusherehekea tukio hili ni sehemu ya harakati za idara, za kuangazia matukio ya kuzaliwa na kufariki kwa Maimamu (a.s), hafla hii imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na mawaidha maalum kuhusu tukio hilo tukufu, yaliyotolewa na mmoja wa wahadhiri wa idara, aliye eleza utukufu wa Imamu Mahadi msubiriwa (a.f), na kujiandaa kifikra na kinafsi katika zama hizi za ghaiba, hafla ikahitimishwa kwa kuimba kaswida na mashairi yaliyo amsha hisia za furaha pamoja na kugawa mauwa”.

Akaendelea kusema: “Hafla hiyo ilipambwa na shindano la kujibu maswali yanayo husu tukio hilo, walioshinda kwa kutoa majibu sahihi wakapewa zawadi, ikafungwa kwa kusoma dua, na kumuomba Mwenyezi Mungu amlete haraka Imamu msubiriwa, na aulinde umma wa kiislamu kote duniani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: