Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa zawadi kwa waliosaidia kufanikisha ratiba ya ziara ya Imamu Askariy (a.s)

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Askariyya umetoa zawadi kwa watu waliosaidia kuhudumia mazuwaru wa Maimamu wawili Askariyyaini (a.s), katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s), miongoni mwao ni watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama sehemu ya kuonyesha thamani ya kazi zao, zilizo anza siku chache kabla ya ziara hiyo.

Hafla ya kutoa zawadi imefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Haadi (a.s) katika Atabatu Askariyya tukufu, na kuhudhuriwa na wawakilishi wake na viongozi wa Ataba hiyo, walio onyesha furaha kubwa waliyonayo uongozi wa Atabatu Askariyya kutokana na msaada waliopewa na nyuso hizo tukufu wa kuwahudumia mazuwaru wa malalo mbili za Askariyyaini (a.s).

Sayyid Hashim Musawi muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na makamo rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya amesema: “Tulithibitisha uwepo wetu na kuhudumia mazuwaru sehemu hii takatifu tangu ilipofunguliwa haram tukufu, hususan kwenye matukio maalum yanayo wahusu Maimamu wawili wa malalo hii takatifu, chini ya maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwenye uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, ambao umekua tayali wakati wote kuchangia kila kinacho hitajika katika utoaji wa huduma”.

Kumbuka kuwa ushirikiano huu sio mgeni, unatokana na kuhisi jukumu la kusaidia kufanikisha ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, na kunufaika na uzowefu wa utendaji wa mambo mbalimbali, chini ya kauli mbiu isemayo (Kuhudumia zaairu ni utukufu kwetu) katika kila mahala linapotajwa jina la Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: