Chuo kikuu Al-Ameed kimeteua wanafunzi waliofaulu

Maoni katika picha
Uondozi wa chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, umeteua wanafunzi waliofaulu kwenye vitivo vyake vya (udaktari, uuguzi, udaktari wa meno), na kupongeza juhudi zao walizofanya wakati wa masomo, na kufaulu kwa kiwango kinacho takiwa na chuo.

Rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maamuzi haya yalifikiwa katika kikao cha mwisho cha baraza la chuo, chini ya maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, yanayolenga kunufaika na vipaji vya wairaq, na kufanya kazi ya kuviendeleza”.

Akaongeza kuwa: “Kufuatia maamuzi hayo, sehemu kubwa ya wahitimu wa kitivo cha uuguzi wa mwaka huu watapewa kazi katika hospitali ya rufaa Alkafeel, tayali hospitali imejiandaa kuwapokea”.

Akabainisha kuwa: “Wanafunzi watakao faulu katika kitivo cha udaktari na udaktari wa meno na famasia, watateuliwa kama walimu wasaidizi kwenye vitivo vya chuo”.

Kumbuka kuwa chuo kikuu Al-Ameed ni taasisi ya kielimu iliyopewa kibali na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, ilifungua chuo binafsi cha kwanza cha udaktari hapa Iraq, chenye vitivo vya (udaktari, famasia, uuguzi, udaktari wa meno), kimekua kituo kikubwa cha elimu, kinachokidhi vigezo vya kimataifa. Kwa maelezo zaidi tembelea toghuti ifuatayo: https://alameed.edu.iq/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: