Familia -Saikolojia- Jamii.. kituo maalum katika Atabatu Abbasiyya kimeanza kutoa ushauri nasaha kwa wahusika kuhudhuria kwenye kikao moja kwa moja

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kuanza kutoa ushauri nasaha kwa wajumbe kuhudhuria kwenye kikao, baada ya kusimama huduma hiyo kwa miaka miwili kutokana na janga la virusi vya Korona, kipichi chote hicho huduma zilikua zinatolewa kwa njia ya mitandao ya mawasiliano ya kijamii.

Mkuu wa kituo bibi Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Chini ya baraka za Mwenyezi Mungu mtukufu tumeanza kutoa ushauri nasaha kwa kuzingatia kanuni za afya, tumeandaa wahudumu waliobobea katika utoaji wa ushauri nasaha katika matatizo yote ya kifamilia, ikiwemo migogoro ya ndoa na wanafamilia, sambamba na mambo ya afya, jamii na saikolojia, na kusaidia familia kutatua migogoro ya watu wake na namna ya kuamiliana nayo”.

Akaongeza kuwa: “Washauri nasaha watakuwepo kila siku kuanzia saa (2 Asubuhi) hadi (saa 8 Adhuhuri), ispokua siku ya Ijumaa, wapo tayali kupokea watu muda wote na kutoa ushauri nasaha bure kwa kutumia njia bora, kiasi cha mshauriwa kupata amani ya nafsi, ushauri nasaha unatolewa katika ofisi ya kituo iliyopo Karbala tukufu/ mtaa wa Mulhaq/ barabara ya hospitali kuu ya Imamu Hussein (a.s)/ jengo la kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s)”.

Akabainisha kuwa: “Ushauri nasaha kwa njia ya mitandao ya mawasiliano ya kijamii utaendelea sambamba na njia ya mahudhurio, tutajibu maswali yote yatakayo tufikia na kutatua matatizo yatakayo wasilishwa kwa njia ifaayo, kupitia namba maalum kwa kila tatizo kama ifuatavyo:

Matatizo ya kisaikolojia:

  • 1- Whatssap 07730134335.
  • 2- Telegram 07730134335.
  • 3- Whatssap 07730242940.

Matatizo ya ndoa:

  • 1- Whatssap 07730242910.
  • 2- Telegram 07730242910.

Matatizo ya watoto:

  • 1- Whatssap 07730242960.
  • 2- Telegram 07730242960.

Matatizo rika:

  • 1- Whatssap 0773024950.
  • 2- Telegram 0773024950.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: