Kituo cha turathi za Karbala kinatoa wito wa kushiriki kwenye kongamano la kimataina na kielimu awamu ya pili

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatoa wito kwa watafiti wote kuja kushiriki kwenye kongamano la kimataifa na kielimu awamu ya pili liitwalo (Harakati za Karbala kielimu katika karne ya kumi hijiriyya).

Litakalo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Turathi zetu ni utambulisho wetu) tarehe 17 – 18 Novemba 2021m, sawa na mwezi 23 – 24 Rabiul-Aakhar 1443h).

Tambua kuwa kongamano litakua na mada tofauti kuhusu turathi za Karbala pamoja na elimu ya Qur’ani, Tafsiri, Hadithi, Fiqhi, Usulu, Falsafa, Aqida, Mantiki, Lugha ya kiarabu, Historia, Uhakiki wa malikale za Karbala na Faharasi.

Linalenga kuangazia harakati za kielimu katika mji wa Karbala karne ya kumi hijiriyya, na kutambulisha wanachuoni wake, hasa wale waliotokea katika zama hizo, sambamba na kuonyesha hazina zilizo andikwa karne hizo na kuendeleza hisia za kielimu kwa watu wa Karbala wa zama tofauti.

Kongamano hili linafanyika wakati kituo kinafanya harakati mbalimbali za kielimu na kitamaduni katika mji wa Karbala, kwa lengo la kuhuisha turathi za Karbala zilizokua na mchango mkubwa katika kuonyesha umuhimu wa mji huu mtukufu na nafasi yake kwenye elimu tofauti na maarifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: