Kitengo cha malezi na elimu ya juu kinaendelea kutoa semina za kuwajengea uwezo watumishi wapya

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatoa semina za kujenga uwezo kwa watumishi wapya wa shule za Al-Ameed.

Semina hizo zinalenga kutambulisha ratiba na mfumo wa ufundishaji unaotumika katika shule za Al-Ameed kwa watumishi wapya, na kufanya vikao vya malezi na elimu katika kitengo cha malezi na elimu ya juu, kwa lengo la kuwaandaa na kuwaingiza kwenye uwanja wa kazi kabla ya kuanza mwaka mpya wa masomo (2021/2022m).

Semina inahusu mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na njia za ufundishaji wa kisasa, mbinu anazoweza kutumia mwalimu anapokua darasani ambazo humpa nafasi mwanafunzi ya kutumia uwezo alionao na kuongeza kipaji chake.

Kumbuka kuwa kitengo cha malezi na elimu ya juu hufanya semina, warsha na mashindano ya kielimu, kwa lengo la kujenga uwezo kwa watumishi wake na kuwaendeleza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: