Kuanza kwa shindano la kuhifadhi Qur’ani tukufu kwa wanawake

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza awamu ya nne ya shindano la kuhifadhi Qur’ani kwa wanawake, ndani ya ofisi za Maahadi katika mkoa wa Najafu, chini ya utaratibu uliowekwa upande wa kuhifadhi na idadi ya majuzuu ya Qur’ani yaliyohifadhiwa, chini ya kamati ya majaji bobezi.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano linaendelea baada ya kusimama siku za nyumba kwa sababu ya janga la virusi vya Korona, shindano hili ni muendelezo wa mashindano yaliyotangulia na matokeo mazuri yaliyopatikana kwa washiriki wake, mashindano haya yanalenga kuandaa mahafidh wa Qur’ani na kuwateua kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa, sambamba na kukomaza uhifadhi wao na kubaini uwezo na vipaji vya usomaji wa Qur’ani”.

Akaongeza kuwa: “Katika siku ya kwanza wamesoma mahafidh kutoka mkoa wa Basra, na tutaendelea kupokea washiriki kwa muda wa siku sita, hadi hatua za mwisho za shindano”.

Akasisitiza kuwa: “Kuna ushindani mkali toka siku ya kwanza, umeshuhudiwa mchuano mkali mbele ya kamati ya majaji, vimejitokeza vipaji vingi vya Qur’ani tukufu, ikiwemo kuhifadhi, sauti na naghma, jambo hilo linatarajiwa kushuhudiwa katika mikoa mingine pia”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake inajukumu la kufundisha elimu ya Dini kwa wanawake, ikitanguliwa na (maarifa ya Qur’ani) na kutengeneza kizazi cha wanawake wenye uwezo wa kufanya tafiti za Qur’ani katika sekta zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: