Kikao cha kwanza cha kongamano la kimataifa Daaru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w) awamu ya pili

Maoni katika picha
Alasiri ya Alkhamisi ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kimeanza kikao cha kwanza cha kuwasilisha mada za kitafiti katika kongamano la kimataifa Daru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w) awamu ya pili.

Mada zilikua na anuani isemayo: (Historia ya Mtume kabla ya Utume), mada sita zimewasilishwa kama ifuatavyo:

  • 1- Kutojua kusoma kwa Mtume (s.a.w.w), imewasilishwa na Dokta Dalali Abbasi kutoka chuo kikuu cha Lebanon.
  • 2- Imani ya wazazi wa Mtume (s.a.w.w) -utafiti katika aya na riwaya- imewasilishwa na Dokta Mukhalad Jabbaar Sultani kutoka idara ya malezi ya Basra.
  • 3- Nafasi ya wahyi katika kuthibitisha Utume wa Muhammad (s.a.w.w), imewasilishwa na Dokta Haidari Taqi Al-Alaaq na Dokta Muhammad Fahadi Alqaisi kutoka chuo kikuu cha Waasitwa.
  • 4- Utafiti wa riwaya zinazopinga utakasifu (umaasumu) wa Mtume (s.a.w.w) kwa Qur’ani na hoja tegemezi, imewasilishwa na Dokta Asgharu Twahamasi kutoka chuo kikuu cha Shahrukurdi.
  • 5- Tabia za Mtume (s.a.w.w) na utekelezaji wa sheria za Mwenyezi Mungu kabla ya Utume, imewasilishwa na Dokta Jafari Muhammad Ayubu kutoka Baharain.
  • 6- Kumtuhumu Mtume (s.a.w.w) na wazazi wake kufanya shirki na kuabudu masanamu, imewasilishwa na Dokta Abdurazaaq Jafari kutoka chuo kikuu cha Basra.

Kikao kikahitimishwa kwa kufungua mlango wa majadiliano na maswali kuhusu mada zilizo wasilishwa, wawasilishaji wakajibu maswali na kufafanua pale palipo hitaji ufafanuzi zaidi.

Kumbuka kuwa kesho siku ya Ijumaa vitafanywa vikao viwili maalum kwa kongamano hili, cha pili na cha tatu na baada ya hapo kutakua na hafla ya ufungaji wa kongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: