Ushiriki wa pekee wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Najafu

Maoni katika picha
Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinashiriki kwenye maonyesho ya vitabu ya kimataifa, yanayo fanywa kwenye uwanja wa maonyesho wa Najafu kuanzia tarehe (20 hadi 30 Oktoba 2021m), kwa ushiriki wa taasisi (200) za usambazaji wa vitabu kutoka ndani na nje ya Iraq.

Katika maonyesho hayo kitengo kinazaidi ya aina (130) za vitabu na majarida, vilivyo tolewa na vituo vilivyo chini yake, sambamba na kuonyesha aina mbalimbali za mbao za hati za kiarabu na michoro ya kiislamu.

Ushiriki huu ni sehemu ya harakati za kitengo cha maarifa, zinazo lenga kuhuisha turathi za kiislamu, kila kinacho onyeshwa na tawi hili kimeandikwa na kuhakikiwa na watumishi wa kitengo hiki.

Tunapenda kusema kuwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, kimeshiriki mara nyingi kwenye maonyesho tofauti ya kitaifa na kimataifa, na mara zote kimekua kikipata muitikio mkubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: