Zaidi ya feni 50 za kunyunyiza maji kwa ajili ya kupoza hewa kwenye maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu zinefungwa

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kila iwezalo kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ili wafanye ibada zao kwa amani na utulivu, imekua ikiboresha huduma zake na kubuni zingine mpya.

Miongoni mwa huduma hizo ni kufunga feni za kunyunyiza maji kwa ajili ya kupoza hewa kwenye maeneo ya wazi, aidha zinasaidia kupunguza ongezeko la joto.

Idadi ya feni zilizo fungwa imefika (55), zimefungwa sehemu zinazo shuhudia msongamano wa mazuwaru, kama vile uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, barabara ya Alqami, barabara ya Baabu-Baqdad, tumeamua kutumia utaratibu huu kwa sababu ndio njia nzuri ya kupoza hewa katika maeneo ya wazi.

Feni zina uwezo wa (120 bar) zimeonganishwa na bomba maalum la maji, umbali kati ya feni na feni ni (mita 7) jumla ya vituo (50) vimewekewa huduma hiyo, pamoja na kituo cha (RO), mita (1050) za waya zimetumika katika mradi huo.

Feni zinafanya kazi kila siku kutokana na kuongezeka kiwango cha joto, kuna kamati maalum ya mafundi inayo simamia mrati huo na kuhakikisha hausimami.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: