Kuhitimisha kongamano la kimataifa Daru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w) awamu ya pili

Maoni katika picha
Alasiri ya Ijumaa mwezi (15 Rabiul-Awwal 1443h) sawa na tarehe (22 Oktoba 2021m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya limehitimishwa kongamano la kimataifa Daru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w) awamu ya pili.

Hafla ya ufungaji imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na kusomwa maazimio ya kongamano, yaliyo somwa na makamo rais wa Daru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w) Dokta Liith Waailiy, kama ifuatavyo:

  • 1- Kusambaza mada zilizo wasilishwa kwenye kongamano kupitia chapisho maalum, kwa ajili ya kutoa nafasi kwa wasomaji na kunufaika nazo.
  • 2- Kufanya awamu ya pili ya shindano la kitabu bora cha historia ya Mtume (s.a.w.w) ili kutoa nafasi kwa wasomi kufanya utafiti wa historia kwa kutumia njia za kisasa.
  • 3- Kuanzisha mtandao wa kielektronik wenye vitabu tofauti vya historia, na kuwa marejeo ya wasomi, watafiti na waandishi.
  • 4- Kuboresha maktaba ya historia kwa kufungua mlango wa kuhakiki nakala kale zinazo husu Mtume (s.a.w.w) na historia yake takatifu, kwa kuhudhurisha nakala kale muhimu na kuzihakiki na kuzichapisha.
  • 5- Kufanya mawasiliano na taasisi za elimu pamoja na vitengo vya historia na lugha ya kiarabu na elimu ya Qur’ani katika vyuo vikuu vya Iraq, kwa ajili ya kufanya nadwa na warsha zinazo husu historia ya Mtume Mtukufu.
  • 6- Kuwa na warsha nyingi za kielimu chini ya wakufunzi waliobobea katika historia na shuhuda za Qur’ani, ili kupata vielelezo vinavyofaa kuonyesha historia kupitia Qur’ani tukufu.
  • 7- Kongamano lijalo litafanywa baada ya miaka miwili Inshallah na litakua na anuani isemayo: (Historia ya Mtume katika vitabu vya tafsiri).

Mwisho watoamada na waliosaidia kufanikiwa kongamano hili wakapewa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: