Muonekano wa furaha: washuhudiwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzaliwa wakweli wawili

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inaipokea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa wakweli wawili Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s), inayosadifu siku ya Jumapili mwezi kumi na saba Rabiul-Awwal, muonekano wa furaha umetanda sehemu zoto za haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Vitengo vinavyo husika na mapambo, vimepamba haram tukufu na kuweka mazingira ya furaha kutokana na tukio hilo takatifu, lenye heshima na hadhi kubwa, kwa nini isiwe hivyo wakati ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu na muongoaji wa umma kipenzi wa Mola wa walimwengu pamoja na kuzaliwa kwa mjukuu wake mkweli wa Aali-Muhammad Imamu Jafari bun Muhammad (a.s).

Kuta za haram tukufu na korido zake zimepambwa vizuri na kuwekwa vitambaa vilivyo dariziwa na kuandikwa maneno mazuri kuhusu mbora wa viumbe Abul-Qassim Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake (a.s), aidha wameweka maua kwenye milango yote ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kuwasha taa za rangi, na kupendezesha mazingira ya kusherehekea mazazi hayo matukufu na kuingiza furaha katika nyoyo za waumini wanaokuja Karbala kuadhimisha kumbukumbu hiyo.

Kumbuka kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) alizaliwa mwezi kumi na saba Rabiul-Awwal mwaka wa tembo, na mjukuu wake Imamu Swadiq (a.s) alizaliwa tarehe sawa na hiyo mwaka wa (80h) na inasemekana (83h).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: