Kazi ya kutengeneza dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) imefika kwenye hatua muhimu

Maoni katika picha
Hatua za kutengeneza dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s), kazi inayofanywa na watumishi wa kitengo cha ufundi wa madirisha ya kwenye makaburi na milango mitukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefika kwenye hatua muhimu, na imepiga hatua kubwa kwa mujibu wa mpango kazi wake, vipande vyake vya madini na mbao vimeanza kukamilika kimoja baada ya kingine, kama ilivyo pangwa na kwa muda uliowekwa, bali sehemu nyingi zimekamilika kabla ya muda, jambo ambalo limeonyesha uzuri wa kazi kwa ujumla.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo Sayyid Naadhim Ghurabi: “Kazi inaendelea katika nyanja mbili, kwanza kutengeneza vipande vya dirisha vya mbao, inahusisha sehemu za juu kwa nje pamoja na nakshi na mapambo ya ndani, kazi hiyo imeanza baada ya kumaliza kutengeneza umbo la mbao, sehemu nyingine ni kutengeneza vipande vya madini, kazi hiyo inaendelea vizuri kama ilivyo pangwa”.

Akabainisha kuwa: “Miongoni mwa hatua muhimu zilizo kamilika na zinazo elekea kukamilika ni:

  • - Kuandika ufito wa maandishi ya Qur’ani, nao ni ufito wa madini ya kopa ulioandikwa surat Insaan yote, nayo yi (Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakua kitu kinacho tajwa) kazi hiyo imekamilika yote ispokua sehemu za kutiwa dhahabu.
  • - Kipande cha ufito wa pambo unaokaa katikati ya maandishi ya Qur’ani na shairi ulionakshiwa kwa mkono herifi ya (S) nayo inajumuisha vipande (14) vikiwa katika mfano wa herufi hiyo, kama ilivyo kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi yote imekamilika ispokua sehemu za kuweka dhahabu.
  • - Ufito wa maandishi ya shairi lililo andikwa na Ali Swafaar Karbalai, lisemalo: (Yeye ni Zainabu binti Hudaa .. bahari ya utukufu na utakatifu), ufito huo pia umekamilika wote ispokua sehemu ya dhahabu”.

Akaendelea kusema: “Miongoni mwa sehemu zinazo endelea vizuri sambaba na sehemu zingine ni vyumba vya madirisha, ambavyo ni sehemu muhimu ya dirisha, kazi hiyo inahitaji umakini na utulivu, kwani inafanywa kwa mikono.

Akamaliza kwa kusema: “Pamoja na tuliyo sema kuna sehemu zingine zenye maendeleo mazuri, kuna zilizo kamilika kama nguzo za pembeni na katikati, nakshi na mapambo yanayo zunguka dirisha, siku zijazo tutaanza kufunga vipande vilivyo kamilika kwenye umbo la dirisha la mbao, kazi inaenda kama ilivyo pangwa, itakamilika kama ilivyo pangwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, mafundi wanafanya kila wawezalo kukamilisha mradi huu kama ilivyo kamilika miradi iliyotangulia, chini ya utendaji wa raia wa Iraq na watumishi wa Ahlulbait Nubuwwah (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: