Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki kwenye maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo endelea hivi sasa linatembelewa na viongozi wengi wa Dini na sekula, miongoni mwa wageni walio tembelea tawi hilo ni makatibu wakuu wa nazaru za kishia hapa Iraq.
Ugeni huo umeangalia vitabu na kusikiliza maelezo kutoka kwa wasimamizi wa tawi hilo, ambao pia wamejibu maswali ya wageni na kufafanua mambo mbalimbali yanayo husu tawi hilo au Atabatu Abbasiyya tukufu, wageni wamefurahishwa na walicho kiona pamoja na uratibu mzuri wa uhakiki, uandishi na uchapishaji, ambao umeongeza uzuri wa tawi, na kuwataka waendelee kushiriki kwenye maonyesho tofauti ya kitaifa na kimataifa, kupitia machapisho tofauti waliyo nayo.
Tambua kuwa ugeni huo ni Sayyid Abdallah Imraan katibu maalum wa mazaru ya Shahidi Aun bun Abdallah (a.s) na Sayyid Alaa Nuri Alkhurasani katibu maalum wa mazaru ya Sayyid Ali bun Hamza (a.s) Karbala, Sayyid Ali Razaaq Wahabi katibu maalum wa mazaru ya Nabii Dhulkifli (a.s).