Mwezi kumi na saba Rabiul-Awwal nuru ya Utume iliangaza duniani kwa kuzaliwa Mtume mtukufu

Maoni katika picha
Mwezi kumi na saba Rabiul-Awwal waislamu wa dunia nzima huadhimisha kuzaliwa kwa mbora wa viumbe mtukufu Muhammad (s.a.w.w), ambaye ni neema kubwa kwa binaadamu, katika zama za ujinga, shirki, masanamu, mwenye nguvu kumnyonya dhaifu, tajiri kumnyanyasa fakiri, katika zama za historia nyeusi yenye upofu wa moyo na ujinga, ardhi ya Maka ilipata jambo la pekee, lililokua halijawahi kutokea katika historia ya wanaadamu kabla yake na wala halitatokea baada yake tukio kama hilo, kwa kuzaliwa rehema ya walimwengu na Mtume wa mwisho Mtukufu Muhammad (s.a.w.w), mwezi kumi na saba Rabiul-Awwal mwaka wa tembo (571) alizaliwa Mtume wetu mtukufu, aliyekuja kupambana na dhulma, ujinga na masanamu, na kurudisha heshima ya mwanaadamu, na kuondoa maisha ya udhalili na ujinga na kuleta maisha ya heshima, utukufu, upendo, kuhurumiana na undugu, Maisha ya tauhidi na kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake bila kumshirikisha na kitu kingine.

Alizaliwa (s.a.w.w) siku ya Ijumaa mwezi kumi na saba Rabiul-Awwal Alfajiri, katika mwaka wa tembo katika mji mtukufu wa Maka, alizaliwa ndani ya nyumba iliyokua ikijulikana kama nyumba ya Muhammad bun Yusufu, nyumba hiyo alipewa Aqiil bun Abu Twalib, watoto wake wakaiuza kwa Muhammad bun Yusufu ndugu wa Hajjaaj.

Wakati wa Haruna Khaizirani aliichukua na kuifanya msikiti, sasahivi msikiti huo ni maarufu watu wanaswali ndani yake na kwenda kuutembelea. Alipewa Utume (s.a.w.w) tarehe ishirini na saba ya mwezi wa Rajabu.

Shekhe Swaduqu amepokea kutoka kwa Abu Abdullah (a.s) anasema: Ibilisi laana iwe juu yake alikua anaenda katika mbingu saba, alipozaliwa Issa (a.s) akazuwiwa kwenda katika mbigu tatu, akawa anaenda katika mbingu nne, alipozaliwa Mtume (s.a.w.w), akazuwiwa kwenda kwenye mbingu zote saba na mashetani wakapigwa kwa vijinga vya moto, Maquraishi wakasema: hiki ndio kiama tulichokua tunasikia watu wa kitabu wanasema.

Amru bun Umayya anasema, naye alikua miongoni mwa watu machachali katika zama za ujinga, angalieni nyota hii ambayo watu huitumia kujua muelekea na muda wa masika na kiangazi, ikianguka kila kitu kitaangamia, na isipo anguka basi ni tukio tu la kupita, asubuhi ya siku aliyo zaliwa Mtume (s.a.w.w) masanamu yote yalianguka chini kwa nyuso zao, jengo la mfalme Kisra likatikisika na vibaraza ishirini na nne vikaanguka, ziwa la Sawa likachafuka na moto wa Farsi ukazimika, ulikua haujawahi kuzimika kwa muda wa miaka elfu moja, Mubadhani katika usiku huo aliota ngamia mkubwa anamuendesha farasi, wakavuka mto wa Dujla na kukatisha eneo ya utawala wa Kisra. Katika usiku huo ilionekana nuru katika miji yote ya Hijazi hadi miji ya mashariki, hakikubaki kitanda cha mfalme yeyote duniani ispokua kilianguka, makuhani hawakujua kitu, uchawi uliharibika, waganga hawakupata mawasiliano ya majini yao, makuraishi walishangazwa sana na tukio hilo, wakaliita ni Aala-Llah, Abu Abdillahi Swadiq (a.s) anasema, waliita Aala-Llah kwa sababu wako katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu.

Amina akasema: Hakika mwanangu alipozaliwa alishika ardhi kwa mikono yake, kisha akainua kichwa na kuangalia mbinguni, halafu ikatoka nuru kwangu iliyoangaza kila kitu, nikasikia sauti ikisema: hakika umezaa mmbora wa watu mpe jina la Muhammad.

Akapelekewa Abdulmutwalib akamchukua na kumuweka miguuni kwake, kisha akasema: Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyenipa mtoto huyu mtukufu, mbora wa watoto, kisha akamuombea dua ya kumlinda kwa utukufu wa nguzo za Alkaaba na akamsomea mashairi, Ibilisi akapiga kelele kuwaita mashetani wenzake, wakakusanyika kwake na kusema: kitu gani kimekusibu ewe kiongozi wetu? Akasema: Ole wenu, mbingu na ardhi vimefungwa tangu usiku, hakika limetokea tukio kubwa sana ardhini, halijawahi kutokea tangu alipoondoka Issa mwana wa Maryam (a.s), nendeni mkaangalie nini kimetokea? Wakasambaa kisha wakarudi na kusema: hatujaona kitu.

Ibilisi akasema: likowapi jambo hilo.

Kisha akapita mbaiwai halafu Jibrilu (a.s) akasema: Una nini Allah akulaani, akasema: naomba kuuliza ewe Jibrilu, kitu gani kimetokea usiku hapa duniani, akamuambia: Amezaliwa Muhammad (s.a.w.w), akasema: Je naweza kupata kitu kwake? Akasema: hapana. Akasema: katika umma wake? Akasema: ndio. Akasema: nimeridhika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: