Watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka idara ya masayyid kitengo cha mahusiano wanapokea mazuwaru kwa kuwapa maua na pipi na maneno ya pongezi katika kumbukumbu ya kuzaliwa nuru mbili ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s).
Jambo hili hufanywa kila mwaka wakati wa kuadhimisha kuzaliwa kwa mbora wa viumbe wote Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambaye ni neema kubwa kwa binaadamu, aliyezaliwa Alfajiri ya mwezi kumi na saba Rabiul-Awwal mwaka wa tembo (571m), sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Jafari bun Muhammad Swaadiq (a.s), hivyo siku hiyo ni tukufu sana, imesuniwa kufanya mambo mengi, miongoni mwake ni kuingiza furaha kwa waumini.
Hivyo watumishi wa malalo takatifu idara ya Masayyid na kitengo cha uhusiano wamesimama milangoni kupokea mazuwaru kwa kuwapongeza na kuwapa pipi tangu asubuhi, kwa ajili ya kuwafanya wahisi umuhimu wa tukio hili tukufu.
Jambo hilo limepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru, wameshukuru kwa kufanyiwa ukarimu huo na kusema pamoja na udogo wa jambo hilo lakini limeacha athari kubwa katika nafsi zao.