Kufanyika kwa kongamano la kuzaliwa Mtume mtukufu awamu ya sita

Maoni katika picha
Chuo kikuu Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya kongamano la sita la kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s) chini ya kauli mbiu isemayo: (Mtume wetu ni kilele cha ubinaadamu).

Kongamano hilo limefanywa ndani ya ukumbi wa kitivo cha famasia, na kuhudhuriwa na rais wa chuo Dokta Nuris Dahani na jopo la wakufunzi, wanafunzi na watumishi, limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyosomwa na mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tawi la Najafu Sayyid Muhandi Almayali.

Ukafuata ujumbe kutoka kwa Shekh Abdullahi Dujaili, akabainisha kuwa: “Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni mtu mtakatifu sana kwetu waislamu, ni kilele cha ubinaadamu, kuadhimisha na kumkumbuka ni kukumbuka misingi bora ya ubinaadamu na maadili mema, sifa aliyokua nayo (s.a.w.w) na iliyomkomboa mwanaadamu kutoka kwenye upotevu hadi kwenye nuru ya rehema na undugu wa ubinaadamu, kuadhimisha mazazi yake kunatufanya tushikamane zaidi na mafundisho yake na kufuata mwenendo wake”.

Pia kulikua na ujumbe kutoka kwa Dokta Ibrahim Juudah, aliye eleza baadhi ya sifa za Mtume (s.a.w.w), akafafanua aya isemayo (Ewe Nabii! Hakika sisi tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na muonyaji * Na mwitaji kumwendea Mwenyezi Mungu kwa idhini yake, na taa lenye kutoa nuru), naye Dokta Muayyad Abdul-Muni’imu akasema: Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuja na Dini inayojali hatua zote anazopitia mwanaadamu, ikiwa ni pamoja na kuleta hukumu kidogo kidogo”.

Baada ya hapo wanafunzi waliopata nafasi za kwanza kwenye masomo yao wakapewa zawadi kama sehemu ya muendelezo wa kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w), aidha kongamano hilo lilipambwa na maonyesho ya picha mbalimbali zilizo chorwa kwa mikono.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: