Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake imeratibu kongamano la kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo: (Kuzaliwa kwa Mtume muongoaji -s.a.w.w- mlango wa rehema), Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imefanya kongamano la kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ndani ya ofisi zake katika mkoa wa Najafu, na kuhudhuriwa na watu wengi.

Kongamano hilo ambalo limekua likifanywa kwa miaka mingi, baada ya kusomwa Qur’ani ya ufunguzi, wanafunzi wa Maahadi wameburudisha masikio ya wahudhuriaji kwa kusoma aya za kitabu kitakatifu, baada ya hapo ndio yakaanza kusomwa mashairi ya kumsifu Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s), na kuahidi kufuata mwenendo wao.

Kisha ikaonyeshwa filamu ya harakati za Maahadi ya Qur’ani tukufu, halafu ukafunguliwa mlango wa kushiriki kwenye shindano la kielimu, ambapo yaliulizwa maswali mbalimbali kuhusu tukio hili, pamoja na kugawa zawadi kwa washindi, mwisho wa kongamano wanafunzi wa Maahadi waliofanya vizuri wakapewa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: