Katika uwanja wa katikati ya haram mbili jana jioni siku ya Jumapili (17 Rabiul-Awwal 1443h) sawa na tarehe (24 Oktoba 2021m), limefanywa kongamano la mashairi kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s) chini ya kauli mbiu isemayo: (Kutoka kwa Muhammad hadi kwa Mahadi ni nuru moja) na kushiriki kundi la washairi na waimbaji.
Katika mazingira yaliyojaa shangwe na furaha jirani na malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), limefunguliwa kongamano kwa Qur’ani tukufu, baada ya hapo washairi wakaanza kusoma mashairi ya kuonyesha mapenzi kwa Mtume (s.w.w.w) na kuonyesha nafasi yake tukufu ya kuongoza watu kuwatoa katika giza la ujinga na upotevu na kuwaingiza katika nuru ya elimu na Imani, sehemu ya kaswida hizo zilihusu kumbukumbu ya kuzaliwa Mkweli wa Aali Muhammad (a.s) Imamu Jafari Swadiq (a.s).
Mahafali hiyo imepambwa na mashairi mengi yaliyo onyesha ukubwa wa mapenzi kwa kiongozi wao Mtume mtukufu (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq na Ahlubait wake (a.s), kwa kufuata muongozo wao na kushikamana nao na kuhuisha utajo wao na mambo yao, pamoja na kuingiza furaha katika moyo wa Imamu wa zama (a.f).