Kufanya shindano la Mtume wa mwisho la usomaji

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya shindano la (Mtume wa mshisho) la usomaji wa Qur’ani na wameshiriki wasomaji ishirini na tano kutoka mikoa tofauti, shindano hili ni sehemu ya kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na limefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s).

Rais wa Majmaa ya Qur’ani Dokta Ahmadi Shekh katika ujumbe Aliotoa kwenye shindano hili amesema, tunalenga kukomaza vipaji vya usomaji, na kuongeza uwezo wa usomaji kwa kufuata hukumu, na kujiandaa kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano makubwa ya kitaifa na kimataifa.

Shindano hilo limesimamiwa na kamati ya majaji iliyoundwa na Ustadh Alaa-Dini Alhamiriy aliye angalia hukumu za usomaji, Shekh Khairi-Dini Ali Alhaadi ameangalia kusimama na kuanza, msomaji Haidari Jalukhani Mussawi ameangalia sauti na nagham.

Shindano lilikua na hatua mbili, hatua ya kwanza ilikua na washindani ishirini na tano, wakafaulu kuingia hatua ya pili washindani sita, kisha yakatangazwa majina ya washindi, mshindi wa kwanza alikua anatoka mkoa wa Baabil, bwana Ahmadi A’araji, na mshindi wa pili anatoka mkoa wa Karbala, bwana Muhammad Kadhim, huku mshindi wa tatu akitoka mkoa wa Najafu, bwana Ahmadi Zaamiliy, mwisho washindi watatu wa mwanzo wakapewa zawadi, na washiriki wote wakapewa zawadi kwa ushiriki wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: