Hafla ya wanawake ya kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Mtukufu

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, linafanya hafla ya kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad na mjukuu wake Imamu Swadiq (a.s), ndani ya uwanja wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na mazuwaru.

Halfa imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na muhadhara uliotolewa na mmoja wa wahadhiri wa idara, akafafanua aya tukufu isemayo (Ewe Nabii! Hakika sisi tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na muonyaji * Na mwitaji kumwendea Mwenyezi Mungu kwa idhini yake, na taa lenye kutoa nuru) amebainisha maana ya taa lenye kutoa nuru, na namna gani Mwenyezi Mungu alivyo angazia ulimwengu kwa kuzaliwa Mtume (s.a.w.w) na akawatoa watu kwenye giza na kuwatia kwenye nuru, na miujiza iliyo onekana siku ya kuzaliwa kwake kama ilivyotajwa kwenye vitabu vitakatifu, kama vile kupigwa mashetani, kutetemeka jengo la Kisra na kuanguka vibaraza ishirini na nne, kuzimika moto wa wafarsi waliokua wanauabudu, kukauka ziwa Sawa, kuanguka masanamu yaliyokua ndani ya Alkaaba tukufu, kutoka nuru kwa Mtume (s.a.w.w) iliyo angaza sehemu kubwa ya uarabuni.

Likafuata onyesho la igizo la tukio la kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w), kisha ukafunguliwa mlango wa kushiriki kwenye shindano la kielimu, halafu washindi wakapewa zawadi, hafla ilipambwa kwa kaswida na mashairi ya kumsifu Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: