Kituo cha kimataifa Al-Ameed ni dirisha kuu la kisekula kwenye maonyesho ya kimataifa ya vitabu yanayo endelea Najafu

Maoni katika picha
Kituo cha Al-Ameed chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeshiriki kwenye maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayofanyika katika Mji wa Najafu kupitia machapisho yake tofauti.

Machapisho ya kituo hicho yamejikita katika mambo ya mazingira, uhandisi, sayansi na lugha ya kiarabu, aidha ni kiunganishi kukuu kati ya kituo na watu wanaokuja kutembelea maonyesho hayo.

Miongoni mwa machapisho yanayo onyeshwa na kituo ni: (jarida la kielimu Albaahir, linalo andika kuhusu elimu ya mazingira na uhandisi), na (jarida la Al-Ameed linalo andika tafiti za kibinaadamu), na (jarida la tasliim linalo andika kuhusu lugha ya kiarabu), na mengineyo miongoni mwa tafiti na vitabu tofauti, vilivyo chapishwa na kituo cha Al-Ameed.

Tambua kuwa hiki ni kituo cha tafiti za kielimu, chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya kazi ya kujenga msingi wa kielimu utakao saidia jamii ya watafiti wa sekula, kinatatua changamoto na kuibua vipawa vinavyo weza kusaidia jamii.

Tambua kuwa kushiriki kwenye maonyesho haya kunasaidia katika kuimarisha mawasiliano na mazuwaru pamoja na kuonyesha machapisho yanayotolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: