Kituo cha turathi za kusini ni dirisha linalo onyesha turathi za mikoa minne

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za kusini ni njia ya kufikia turathi za mikoa minne ya kusini ambayo ni (Dhiqaar, Misaan, Diwaniyya na Muthanna), nacho ni moja ya vituo vya kitafiti vilivyo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Tumeongea na mkuu wa kutuo hicho Dokta Hussein Sharhani kuhusu huduma zinazo tolewa na kituo hicho amesema: “Kituo kinajukumu la kukusanya turathi za mikoa minne, hususan turathi za kidini, kielimu, kitamaduni na kijamii”.

Akaongeza kuwa: “Kituo baada ya kufanya kazi mfululizo kupitia walimu wa chuo kikuu cha Dhiqaar na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kazi hizo ziliishia kupendekeza kufungua kituo cha turathi za kusini, kitakacho jihusisha na turathi za mikoa tuliyotaja”.

Akaendelea kusema: “Kituo chetu ni muendelezo wa vituo vilivyo funguliwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu vilivyopo kwenye mikoa tofauti, kwa lengo la kutunza turathi, kuzihakiki na kufanya tafiti za mambo mbalimbali, kwa sababu zinauwiana na tamaduni za jamii, pia ni msingi unaotujulisha vizazi vilivyo tangulia”.

Mkuu wa kituo akasema: “Kituo kilianzishwa tarehe (15/12/2018m), kikaanza kazi tarehe (22/9/2019m) kwa kukusanya turathi za mikoa ya kusini”.

Akafafanua kuwa: “Kituo kina idara zifuatazo: (idara ya uhakiki, idara ya utafiti, idara ya habari, idara ya toghuti na maktaba, idara ya rasilimali watu na utumishi, idara ya mawasiliano na ufuatiliaji), idara zote zinafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa”.

Tambua kuwa vituo vilivyo chini ya kitengo cha maarifa ni: (kituo cha turathi za Karbala, kituo cha turathi za Hilla, kituo cha turathi za Najafu, kituo cha turathi za Basra, kituo cha turathi za kusini, kituo cha tafiti za kiislamu kilichopo Mash-had takatifu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: