Riyaadhu-Zaharaa daima inakuwepo katika maonyesho ya vitabu

Maoni katika picha
Machapisho mbalimbali ya Atabatu Abbasiyya tukufu, yanalenga tabaka tofauti za jamii yanashiriki katika maonyesho ya vitabu ya kitaifa na kimataifa, na jarida la Riyaadhu-Zaharaa (a.s) linalo chapishwa na maktaba ya Ummul-Banina (a.s) limepata muitikio mkubwa kutoka kwa watu wanaotembelea maonyesho ya vitabu yanayo endelea hivi sasa katika mkoa wa Najafu.

Watu wanaotembelea tawi letu katika maonyesho haya wanapata wanacho hitaji kwenye jarida hili ambalo hutolewa kila mwezi, kupitia maudhui zake zinazo husu mwanamke wa kiislamu, sambamba na kujenga uwezo wa wanawake kidini na kitamaduni, maudhui zake zinaeleza mambo halisi sio mambo ya kufikirika, sambamba na kuweka utatuzi wa kila changamoto anayokutana nayo mwanamke.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki kwenye maonyesho hayo ya kimataifa, ambayo taasisi (200) za usambazaji wa vitabu zimeshiriki kutoka ndani na nje ya Iraq, Ataba imewakilishwa na kitengo cha Habari na utamaduni, kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, wakiwa na shehena kubwa ya vitabu vya aina mbalimbali, tawi limepata muitikio mkubwa kutoka kwa wadau wa maonyesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: