Kitengo cha Dini kinafanya kazi kubwa ya kuhudumia jamii

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya kazi kubwa ya kufundisha jamii, kwa kutegemea maarifa na misingi ya sheria za kiislamu.

Kuhusu huduma zinazotolewa na kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, rais wa kitengo hicho Shekhe Swalahu Khafaji ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kitengo cha Dini kinajitahidi kufanyia kazi mahitaji ya mazuwaru kiroho pamoja na mambo mengine”, akaongeza kuwa: “Wahudumu wetu Masayyid na Mashekhe watukufu wanawasilisha maoni ya kifiqihi, na maelekezo ya Maraajii Dini katika mambo mbalimbali ya kimaisha, hususan hukumu za mambo tofauti katika Maisha ambayo ni muhimu kwa kila mtu kuyafahamu katika jamii ya kiislamu”.

Akaendelea kusema: “Miongoni mwa harakazi zingine zinazofanywa na kitengo cha Dini ni kusambaza mafundisho ya Ahlulbait (a.s) na kutambulisha utukufu wao na kuonyesha nafasi yao ambayo kila anayeamini ukuu wao (a.s) anatakiwa kutambua”.

Akasema: “Kazi hiyo hufanywa kupitia mimbari zilizopo ndani ya haram tukufu, hutumika kueleza utukufu wa Ahlulbait (a.s) na misiba yao na namna walivyo zulumiwa haki zao na kundi la watu waliopotea, mambo hayo huwa na muitikio mkubwa hasa wakati wa mwezi wa Muharam na Safar”.

Akasisitiza kuwa: “Kazi za kitengo hiki hazijajikita sehemu moja peke yake ndani ya haram tukufu au mji wa Karbala, bali kuna ratiba ya kuwasiliana na jamii katika mikoa tofauti ya Iraq, na kushirikiana nao kwenye shida na raha, kwa kutoa misaada ya kimaana na kimaada kutoka idara kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya kiongozi mkuu wa kisheria na katibu mkuu”. Akasema: “Kamati ya misaada katika kitengo cha Dini ilikua na nafasi kubwa wakati wa vita dhidi ya makundi ya kigaidi, bado kamati hiyo inafanya kazi ya kuwasiliana na wapiganaji waliopo kambini”.

Akakumbusha: “Kuna baadhi ya harakati zinaendelea kila siku, ikiwa ni pamoja na kufungisha ndoa na kusimamia viapo vya kisheria, kwa ajili ya kuondoa mizozo baina ya watu, na kujaribu kuwaweka karibu na kuondoa tofauti katika jamii, kwa ajili ya kueneza usalama na kujiepusha na ugonvi ambao husababisha hasara kwa mtu na jamii”.

Tambua kuwa kitengo cha Dini kinaharakati nyingi, hufanywa sambamba na ratiba za Atabatu Abbasiyya tukufu ndani na nje ya mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: