Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel imepokea wanafunzi 100 kutoka mkoa wa Basra

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel katika idara ya watoto na makuzi chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imepokea wanafunzi (100) wenye viwango tofauti na wanaoshiriki kwenye miradi tofauti ya kijamii hapa Iraq, kutoka katika mkoa wa Basra, wameandaliwa ratiba maalum yenye vipengele vingi.

Kiongozi wa idara katika ofisi ya watoto Ustadh Ali Hussein Abduzaidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel imekua ikifanya kazi kubwa ya kuhudumia tabaka la vijana, kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwatumia kwenye shughuli za kitamaduni, kielimu na michezo”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba imepangwa kwa kushirikiana na mradi wa utamaduni wa vijana wa Iraq, katika mji wa Imamu Hussein (a.s) chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu, wamefundishwa masomo ya idikadi ya kiislamu, makuzi na utamaduni, aidha kulikua na michezo na mashindano mbalimbali, ratiba hiyo imesimamiwa na kuendeshwa na walimu mahiri”.

Akabainisha kuwa: “Wanafunzi tuliopokea ni wale walioshiriki katika miradi tuliyofanya katika mkoa wa Basra, kuwakaribisha hapa ni sehemu ya kupongeza kuzi nzuri walizo fanya siku za nyumba, mwisho wa ratiba tumegawa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mambo mbalimbali, tunawatakia mafanikio mema wote kwa ujumla katika maisha yao ya kielimu na kikazi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: