Jarida la (Atwaau-Shabaab) linalo tolewa na kituo cha utafiti na ubunifu chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, vijana wamevutiwa nalo sana katika maonyesho ya vitabu yanayo endelea mjini Najafu, kutokana na uzuri wa mada zake zinazo eleza tabaka la vijana katika jamii, pamoja na kutaja changamoto wanazo kutana nazo na kuonyesha utatuzi wake.
Jarida linaumuhimu mkubwa bila kusahau umuhimu wa kundi lengwa, ambalo ndio kundi muhimu katika jamii, linaelekeza fikra zao na kuwaongoza katika mambo yenye manufaa kwao, pamoja na kuelekeza jinsi ya kupambana na changamoto za maisha, na kusisitiza umuhimu wa ubunifu kwani wao ndio msingi wa jamii, hivyo jarida hili ni muhimu kwa familia kutokana na maudhui zake na uwasilishaji wa mada zake katika mitazamo tofauti.
Kutokana na tuliyo eleza wasimamizi wa maonyesho, wamehakikisha jarida hilo linashiriki kwenye maonyesho haya, kwa ajili ya kupata maoni ya vijana na ushauri wao, katika kujenga vijana wabunifu na kutimiza ukuaji wa akili, roho na mwenendo.
Jarida linamilango mbalimbali, ambayo imelifanya kuwa na upekee wa aina yake kwa tabaka la vijana na kuwa karibu nao zaidi, jambo hilo limethibitishwa na wadau wake.
Tambua kuwa jarida la Atwaau-Shabaab hupokea maoni na ushauri kutoka kwa wasomaji wake, na linawasiliana nao moja kwa moja kupitia ukurasa wake wa (facebook) au barua pepe ifuatayo: (info@alkafeel.net) au (ataa@alkafeel.net).