Kituo cha turathi za Hilla kinafanya mkutano wa kumi na moja

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Hilla kinafanya mkutano wa kumi na moja wenye anuani isemayo (ufaulu wa tafsiri kwa wanachuoni wa Hilla kuanzia karne ya sita hadi kumi hijiriyya), na kuhudhuriwa na wasomi wa hauza na sekula.

Katika mkutano huo Dokta Mithaaq Abbasi Alkhafaji amewasilisha utafiti wake, ambapo ameeleza upekee wa Hilla katika tafsiri kupitia wanachuoni wake watukufu, akaanza kwa kutoa takwimu ya idadi za aya alizotolea ushahidi na kutaja wanachuoni muhimu waliobobea katika uwanja wa Qur’ani.

Baada yahapo washiriki wa mkutano wakapewa nafasi ya kuuliza maswali sambamba na kikao hicho kupambwa na mashairi kutoka kwa Muhammad Abdulmuhsin Sha’abith.

Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Hilla kipo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya kazi kubwa ya kuhuisha turathi za mji wa Hilla kupitia machapisho yake na harakati tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: