Kufungua mlango wa usajili katika semina ya (njia ya mafanikio) kwa wanawake

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefungua mlango wa usajili kwa watakaoshiriki kwenye semina ya (njia ya mafanikio) kwa wasichana wenye umri tofauti, semina itaendeshwa kwa njia ya kuhudhuria moja kwa moja darasani (sio kwa njia ya mtandao) madarasa yapo katika jengo la Swidiqatu-Twahirah/ mtaa wa Mulhaqu/ barabara ya Hospitali ya Imamu Hussein (a.s).

Mkuu wa kituo hicho bibi Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Usajili unafanywa kupitia link ifuatayo: t.ly/K76D ratiba itakua kama ifuatavyo:

Mada za semina:

  • 1- Kujitanbua na mchango wake katika mafanikio.
  • 2- Athari ya fikra mbaya katika mafanikio.
  • 3- Athari za kutosheka katika maisha, elimu na kazi”.

Akaongeza kuwa: “Semina inalenga kueleza mafanikio ya wanawake na itaendeshwa na wasomi waliobobea katika sekta hiyo, sambamba na kubainisha hatua sahihi za mafanikio”.

Kumbuka kuwa kituo cha utamaduni wa familia kinahusika na mambo ya familia, kilianzishwa kwa lengo la kufundisha maadili mazuri katika familia za raia wa Iraq na kutatua mizozo ya kifamilia, pamoja na kujenga utulivu wa nafsi katika familia, kinafanya kazi ya kuhudumia wanafamilia na kufuatilia maendeleo yao, chini ya mkakati maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: