Ugeni kutoka Ataba mbili tukufu umewasili Miqdadiyya na kuhudhuria maombolezo ya mashahidi wa Kijiji cha Rashaad

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya siku ya Ijumaa mwezi (22 Rabiul-Awwal 1443h) sawa na tarehe (29 Oktoba 2021m), umehudhuria kikao cha kuomboleza mashahidi wa Kijiji cha Rashaad katika mji wa Miqdadiyya waliofariki katika shambulio la kinyama lililofanywa na magaidi wa Daesh na kufariki watu (15) na wengine (17) majeruhi.

Ugeni huo umehusisha viongozi wa Ataba mbili na watumishi wake, wamewasilisha rambirambi za Marjaa Dini mkuu na viongozi wakuu wa kisheria pamoja na watumishi wa Ataba mbili tukufu kwa familia za mashahidi na wahanga.

Muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika ugeni huo Shekhe Aadil Wakiil ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na maelekezo ya viongozi wakuu wa kisheria wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, leo tumefika kutoa pole kwa familia za mashahidi waliouawa bila hatia yeyote kufuatia shambulizi la magaidi, na tumewasilisha rambirambi kwa ndugu wa mashahidi na kumuomba Mwenyezi Mungu awaweke mahala pema peponi mashahidi watukufu na awape subira na uvumilivu ndugu wa mashahidi na majeruhi awaponye haraka”.

Akaongeza kuwa: “Kuja kwetu kutoa pole kwa familia hizi ni sehemu ya harakazi zinazo fanywa na Ataba mbili tukufu katika jamii ya Iraq, ikiwa ni pamoja na kuja kuwafariji wakazi wa mkoa huu ambao wamekua wahanga wakubwa wa mashambulizi ya magaidi, na kutoa mashahidi wengi ambao wamekua ngao imara ya kuzuwia njama za magaidi”.

Kumbuka kuwa Kijiji cha Rashaad kilichopo kusini magharibi ya mji wa Miqdadiyya, jioni ya Jumanne iliyopita lilitokea shambulio la kinyama, lililofanywa na magaidi wa Daesh na kusababisha vifo vya watu (15) na majeruhi (17) wote wanatokana na kabila la bami Tamiim.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: