Kuanza ratiba ya (Naafidhu-Albaswirah)

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni Multaqal-Qamaru chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaanza ratiba ya (Naafidhu-Albaswirah) inayo lenga watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ratiba yenye vipengele vingi tofauti, itadumu kwa muda wa siku tatu, itakua chini ya usimamizi wa watumishi wa kituo hicho.

Kiongozi wa kituo Shekh Haarith Daahi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ratiba hii imeandaliwa kwa maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kutekelezwa na uongozi wa kitengo, watumishi watashiriki kwa hiyari, sambamba na kuzingatia aina ya masomo yatakayo tolewa na kitengo cha mshiriki, kwa lengo la kujenga uwezo wake na kuboresha huduma zinazo tolewa kwa mazuwaru wa malalo takatifu”.

Akaongeza kuwa: “Jina la ratiba hii ni moja ya sifa za Abulfadhil Abbasi (a.s), linakumbusha wajibu wa watumishi na kujituma katika kutekeleza majukumu yao kama yalivyo pangwa katika vitengo vya Atabatu Abbasiyya, na tunatarajia kuwafikia watumishi wengi kadri itakavyo wezekana, miongoni mwa mambo yaliyopo kwenye ratiba ni:

  • - Kutengeneza lengo kuu.
  • - Majadiliano kuhusu uhakika wa Dini.
  • - Makosa ya kimtandao.
  • - Kujenga mazowea.
  • - Utata wa zama hizi.
  • - Kufuata na kujitahidi.
  • - Kutii taasisi mbili.
  • - Njia za kufuata katika kutatua migogoro na mbinu za mazungumzo.

Pamoja na mihadhara ya kujenga uwezo na vikao vya majadiliano ya wazi kwa wote na vipindi vya mapumziko”.

Akamaliza kwa kusisitiza kuwa: “Mambo tuliyo chagua katika ratiba hii, yamechaguliwa kwa umakini mkubwa na tunaamini yatasaidia kujenga uwezo wa mtumishi, na yanaendana na mazingira halisi ya kazi aidha tunatekemea kuwa na matokea mazuri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: