Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake imehitimisha moja ya semina za kuhifadhi kitabu kitakatifu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imehitimisha semina ya kuhifadhi Qur’ani tukufu.

Makamo kiongozi mtendaji wa Maahadi Dokta Janaan Ghaalib amesema: “Hakika ni furaha kubwa wanafunzi wetu kumaliza kuhifadhi Qur’ani tukufu, sambamba na kusoma kwa usahihi na kuchunga hukumu za usomaji”, akaongeza kuwa: “Maahadi inaendelea kusaidia wanafunzi kwa kuwapa walimu watakao endelea kuwasikiliza na kukomaza uhifadhi wao wa Qur’ani tukufu na kuwafanya kuwa tayali kuwakilisha Maahadi wakati wowote kwenye mashindano ya Qur’ani tukufu”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani inalenga kusambaza elimu ya Dini kwa wanawake, ikiongozwa na (Somo la Qur’ani), na kuandaa kizazi cha wanawake wasomi wenye uwezo wa kufanya tafiti katika sekta zote za Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: