Mapokezi makubwa ya maukibu ya watu wa Karbala katika mkoa wa Waasit

Maoni katika picha
Maukibu ya watu wa Karbala inayo shiriki katika maombolezo ya kifo cha Taabii Saidi bun Jubair (r.a) imepata mapokezi makubwa, katika malalo yake iliyopo wilaya ya Hai kusini mwa mkoa wa Waasit, imefanywa kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Mapokezi hayo yameongozwa na mkuu wa mkoa wa Waasit Dokta Muhammad Jamili Almayahi, kaimu mkuu wa wilaya ya Hai na mkuu wa polisi pamoja na viongozi wengine, zimesomwa kaswida na semi za makaribisho, mkuu wa mkoa ameikaribisha maukibu kwa kutumia maneno mazuri.

Aidha kulikua na ujumbe uliowasilishwa na rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan, ameshukuru makaribisho mazuri waliyopewa, ambayo ni desturi ya watu wa mkoa huu na wilaya hii kuwakaribisha waombolezaji kutoka Karbala namna hii, pia kulikua na ujumbe wa Hussein Mankushi kaimu kiongozi wa Karbala ulio wasilishwa kwa niaba yake, ulioanza kwa kutoa salamu za watu wa Karbala kwa watu wa Hai.

Maukibu itashiriki katika shughuli za uombolezaji, Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimejitolea magari ya kubeba waombolezaji kutoka Karbala hadi kwenye malalo ya Saidi bun Jubairi (r.a), na kitengo cha maadhimisho na mawakibu kimewasiliana na mamlaka zinazo husika kwa ajili ya kufanikisha zowezi hili, ambalo hufanywa kila mwaka katika siku kama hizi za kuomboleza kifo cha Taabii huyu mtukufu aliyefariki mwezi ishirini na tano Rabiul-Awwal.

Kumbuka kuwa Saidi bun Jubair (a.r) ni katika wafuasi wa Imamu Zainul-Aabidina (a.s) alikua mwanachuoni mkubwa na mashuhuri katika somo la Fiqhi na Tafsiri, aliuawa na Hajjaaj bun Yusufu Athaqafii kwa sababu ya kuungana na Abdurahmani bun Ash’ath dhidi ya bani Umayya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: