Watu wa Karbala wanaomboleza kifo cha taabii Saidi bun Jubair (r.a)

Maoni katika picha
Maukibu ya watu wa Karbala kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya jioni ya Jumamosi mwezi (23 Rabiul-Awwal 1443h) sawa na tarehe (30 Novemba 2021m) wameomboleza kifo cha taabii (mtoto wa swahaba) Saidi bun Jubair (r.a) mbele ya malalo yake iliyopo wilaya ya Hai kusini mwa mkoa wa Waasit.

Rais wa kitengo ambaye ni miongoni mwa waliokuwepo katika maukibu hiyo ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kuhuisha ukumbusho huu ni miongoni mwa matukio ambayo maukibu hii imezowea kuyafanya, Ataba mbuli tukufu zimejitolea magari ya kubeba wanachama wa maukibu, wanaotokana na vikundi tofauti vya watu wa Karbala”.

Akaongeza kuwa: “Kama kawaida, matembezi ya maukibu hiyo yamefanywa kwa vikundi, na wakati wa matembezi hayo wameimba kaswida za Husseiniyya zilizo amsha hisia za majonzi ya msiba huo, walipo ingia katika haram yake tukufu wakafanya majlisi ya kuomboleza, ambapo kaswida na tenzi mbalimbali zimesomwa, zilizo eleza matatizo waliyopata wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wakiwemo maswahaba wakubwa na Taasii Saidi bun Jubair (r.a)”.

Tambua kuwa malalo ya Taabii Saidi bun Jubair (r.a) imeshuhudia kuwasiri kwa maukibu nyingi za waombolezaji wa msiba huu, miongoni mwa maukibu hizo ni hii ya watu wa Karbala, kitengo kimefanya taratibu zote za uombolezaji huu, hii sio mara ya kwanza kufanya tukio hili mbele ya malalo hii takatifu, bali limekua likifanyika kila mwaka, ni jambo ambalo watu wa mkoa huu wamelizowea na kurithishana.

Kumbuka kuwa Taabii Saidi bun Jubairi (r.a) ni miongoni mwa wafuasi wa Imamu Zainul-Aabidina (a.s), alikua ni miongoni mwa wanachuoni mashuhuri wa Fiqhi na Tafsiri, Ibun Abbasi alikua anapoendewa na watu wa kufa kuulizwa maswali anasema: Hayupo kwenu ibun Ummu Dahmaau? Yaani Saidi bun Jubair, alikua anaitwa mjuzi wa wanachuoni, alikua anafundisha msikitini baada ya Alfajiri na baada ya Al-Asri, aliuawa na Hajjaaj bun Yusufu Athaqafii, kwa sababu ya kuumgana na Abdurahmani bun Ash’ath katika vita dhidi ya bani Ummayya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: