Semina ya kujenga uwezo katika uhandisi, idara na viwanda

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeratibu semina ya kukuza uwezo katika uhandisi, idara na viwanda, kwa kulenga watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Semina imedumu kwa muda wa siku tatu ndani ya jengo la Alhaad (a.s) chini ya ukufunzi wa wasomi wa sekula, walio wasilisha mada tofauti ikiwemo uhandisi, idara, viwanda, utafiti wa kiuchumi na vifaa vya kiofisi na kihandisi na ubora unaokubalika.

Semina inalenga kujenga uwezo wa watumishi wanaoendesha miradi ya kihandisi na viwanda chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kuzingatia ubora wa kimataifa sambamba na:

  • - Kutambua ubora na hatua zake.
  • - Kutambua utawala bora na sekta zake.
  • - Kutambua utaratibu wa ISO.
  • - Kutambua misingi ya utawala bora.
  • - Kutambua sifa za kipimo cha kimataifa cha (ISO9001:2015).

Tambua kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya kila iwezale kujenga uwezo wa watumishi wake wa fani tofauti, hivyo hufanya warsha na semina za kielimu kila wakati.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: