Atabatu Abbasiyya tukufu inafunga ushiriki wake katika maonyesho ya vitabu kimataifa yanayo fanyika Najafu

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inafunga ushiriki wake katika maonyesho ya vitabu chini ya anuani isemayo: (Najafu mazingira na kitabu) yamedumu siku kumi, jumla ya nchi (14) za kiarabu na kiajemi zimeshiriki, na taasisi za usambazaji wa vitabu (200) zikiwa na zaidi ya aina (250) za vitabu.

Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu lilikua muhimu kwenye maonyesho hayo, nalo liliundwa na kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, hakika tawi hili limevutia wadau wengi wa maonyesha haya, kutokana na kuwa na vitabu vya aina tofauti (Dini, utamaduni, sekula, historia, falsafa, Qur’ani, Watoto, utamaduni wa mwanamke) na vinginevyo, kwa mujibu wa kauli za waliotembelea tawi hili wamesema lilikua la pekee.

Shelfu za tawi zilipambwa na aina (450) za vitabu vya aina tofauti yakiwemo majarida, kitengo cha habari na utamaduni kilikua na zaidi ya vitabu (360) na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kilikua na aina (130), vitabu vyote ni kazi ya waandishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na vimechapishwa na Ataba, hili ni jambo la pekee halipatikani kwa wengine.

Rais wa kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maonyesho haya yamepata muitikio mkubwa, jambo hili linaonyesha kukubalika kwa vitabu vilivyo onyeshwa, aidha ni nafasi ya wadau kuangalia maendeleo ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Ushiriki wa maonyesho haya unaumuhimu mkubwa, kwani ni mara ya kwanza kufanywa maonyesho ya kitaifa kama haya katika mji wa elimu na wanachuoni wa Najafu Ashrafu, wamekutana makumi ya maelfu ya wasomi, waandishi, watafiti na wasambazaji wa vitabu kutoka nchi za kiarabu na kiajemi, watu waliotembelea maonyesho haya wameshuhudia turathi kubwa ya elimu na utamaduni”.

Kumbuka kuwa maonyesho yalifunguliwa tarehe ishirini mwezi wa kumi, nchi zifuatazo zimeshiriki: Misri, Sirya, Lebanon, Jodan, Iran, Falme za kiarabu, Saudia, Sudani, Uingereza, India, Tunisia na Qatar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: