Mkuu wa kitengo cha uchapishaji Ustadh Farasi Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na mafanikio ya uchapaji yaliyopatikana, wizara ya malezi imeweza kutekeleza jukumu lake la kuchapa vitabu vya kufundishia, tena vyenye ubora mkubwa katika kila msimu wa masomo, tumefanikiwa kuchapa vitabu kwa utaratibu wa (Art Matt) mara ya kwanza, kwa kutumia karatasi nzuri zenye rangi yenye muonekano mzuri”.
Akaongeza kuwa: “Kiwanda kimekamilisha makubaliano yote tuliyofanya na wizara ya malezi, miongoni mwa makubaliano hayo ni kufanya tafiti katika hatua tofauti, ukweli na ubora ndio kauli mbiu yetu na tumeweza kuithibitisha kwa vitendo”.
Akasisitiza kuwa: “Miongoni mwa sababu kubwa za wizara ya malezi kuchapisha vitabu vyake katika Daarul-Kafeel, ni mafanikio yaliyopatikana na upanuzi wa kazi ya uchapaji ambayo imekua na wateja wengi miongoni mwa taasisi na watu binafsi, machapisho yake yote yanakidhi sifa za kimataifa”.
Akabainisha kuwa: “Uchapaji wetu unazingatia mambo mengi, miongoni mwake ni:
- - Ubora wa karatasi miongoni mwa zile zinazotengenezwa Ulaya, ni rafiki kwa mazingira na zinashikika vizuri.
- - Rangi zake zinamvuto mzuri na herufi zinaonekana viruri.
- - Vimejaladiwa vizuri na rahisi kwa mwanafunzi kufunua, ni imara zinadumu kwa muda mrefu.
- - Maandishi yanamuonekane mzuri na hati na michoro vinaonekana vizuri na hiyo inatokana na ubora wa mitambo ya uchapishaji.
- - Kila kitabu kinaunganishwa na kutengenezwa kulingana na ukubwa wa kitabu na idadi za karatasi zake”.