Ushiriki wa pekee wa kituo cha faharasi na kupangilia taaluma katika shughuli za kongamano la Multaqal-Arabi la kupata uhuru

Maoni katika picha
Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma kimeshiriki katika shughuli za kongamano la Multaqal-Arabi awamu ya pili, lililohitimishwa hivi karibuni nchini Tunisia chini ya uratibu wa taasisi ya kiarabu ya malezi utamaduni na elimu (idara ya Ako) Umoja wa waarabu wa kupata uhuru (Teknolojia ya taaluma na mawasiliano).

Kituo kimeshiriki kwenye kongamano hilo kupitia mada mbili:

Ya kwanza ilikua inasema: (Semina za kielimu zinazotolewa na mtandao wa kimataifa Alkafeel na nafasi yake katika mawasiliano ya kielimu), iliwasilishwa na Ustadh Hasanain Najmu Abdu na Ustadh Mustwafa Yusufu Hussein.

Mada ya pili inasema: (Majarida ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika kapu la majarida ya kisekula na kielimu ya Iraq kwa mtazamo wa wanufaika..), imewasilishwa na Ustadh Hussein Muhammad Ibrahim Hassan na Ustadh Sefu Abdul-Amiir.

Ushiriki ulikua mzuri na mada zimekubalika kwa wahudhuriaji zaidi ya (500) kutoka kila upande wa dunia, kongamano lilikua na vikao sita ambapo jumla ya mada (30) zimewasilishwa, na vikao viwili vya wazungumzaji wakuu, aidha kulikua na meza mbili za duara na mipango kazi sita iliyogawanywa kwa idadi ya siku.

Mwisho wa kongamano likawasilishwa tamko la (azimio la kiarabu kwa elimu huru) lililokua na mapendekezo kadhaa yaliyotolewa kwa taasisi za kitafiti, kielimu, kiserikali na wanasiasa pamoja na viongozi tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: