Mashamba ya Atabatu Abbasiyya tukufu yameanza mavuno ya msimu huu

Maoni katika picha
Kitengo cha kilimo na ufugaji chini ya shirika la biashara Alkafeel ambalo ni moja ya mashirika ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimesema kuwa mashamba yake yameanza yameanza kutoa mazao ya msimu kwa soko la ndani, tayali wameanza kuingiza mazao hayo sokoni na kusaidia kuondoa haja ya kununua mazao nje ya nchi.

Rais wa kitengo hicho Mhandisi Ali Muz’ali Laaidh, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa kipaombele sana katika sekta ya kilimo, kwa lengo la kukuza sekta hiyo na matumizi bora ya Ardhi, na kuongeza bidhaa zinazozalishwa ndani na kuacha kutegemea bidhaa zinazotoka nje ya nchi, na kusaidia kujenga uwezo wa kujitegemea, pamoja na kutoa ajira kwa watu wengi katika sekta hii muhimu”.

Akaongeza kuwa: “Mazao yanayolimwa ni yale ambayo mwananchi anayahitaji siku zote, kama: (Nyanya za aina mbalimbali, bilinganya, viazi mbatata, tango, pilipili baribi na kali, kabichi ya kijani na nyekuni, riyam, vitunguu vyekundu vya njano na vyeupe), mazao hayo yamelimwa katika green house (4) kubwa, kila moja inaukubwa wa mita za mraba (5000) na kuna green house ndogo (95) kila moja inaukubwa wa mita za mraba (516) pamoja na maeneo mengine, akasisitiza kuwa: “Mazao yanayo zalishwa yanaubora mkubwa, kwani hayatumii mbolea zenye kemikali (ipm), mbolea inayotumika ni ya asili, inayo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud, mbolea hiyo ni rafiki kwa mazingira na inauwezo mkubwa, mazao yanakua na radha nzuri, na inazuwia maradhi ya mimea na inaendana na mazingira ya Iraq, imekua msaada mkubwa wa kuongeza mazao katika soko la Iraq”.

Mhandisi Falahu Fatli mkuu wa kitengo cha masoko katika shirika la Khairul-Juud amesema kuwa: “Sifa ya pekee inayopatikana katika mashamba ya Atabatu Abbasiyya tukufu, mazao yake yanaradha nzuri inayotokana na kutumia aina bora kabisa ya mbolea na kufuata utaratibu wa kilimo cha kisasa, katika umwagiliaji, usamadiaji, ujenzi wa green house na kuweka mazingira mazuri ya ukuaji wa mimea, pamoja na kuwepo kwa wataalamu waliobobea na wenye uzowefu mkubwa katika sekta hii, mashamba haya ni sehemu ya mashamba darasa yenye mafanikio makubwa”.

Kumbuka kuwa mashamba haya ni mfano hai wa kubadilisha ardhi ya jangwa kuwa kijani kibichi na sehemu bora ya kilimo, nayo ni mashamba ya kisasa yaliyowekwa miundombinu bora na yakisasa kabisa duniani, mazao yanayopatikana katika mashamba hayo ni mazuri kwa lishe na rafiki wa mazingira na yanasaidia kwa kiwango kikubwa soko la Iraq katika kila msimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: