Kongamano la kujadili mkakati wa kuhifadhisha Qur’ani tukufu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani tukufu, imefanya kongamano la wazazi wa wanafunzi wanaohifadhi Qur’ani, chini ya kauli mbiu isemayo: (Qur’ani tukufu ni msingi wa itikadi na ngao ya jamii), ndani ya ukumbi wa Shekh Answaari (r.a) kwenye jengo la Imamu Almurtadha (a.s) mkoani Najafu, kwa anuani isemayo: (Kuboresha mazingira ya kujifunza kwa mahafidhu).

Kongamano limehudhuriwa na jopo la wataalamu lililoundwa na Maahadi, kwa lengo la kuendeleza mradi wa kuhifadhi Qur’ani tukufu, na kikosi kazi kinacho simamia kuhifadhisha Qur’ani katika Maahadi, kikao hiki kimefanywa kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha mazingira ya kujifunza mahaafidh, sambamba na kuweka uhusiano mzuri kati ya Maahadi na wazazi, na kujadili kwa pamoja mkakati wa kuhifadhisha Qur’ani tukufu kwa kuangalia (chanya na hasi zake), na kutambua changamoto kubwa wanazopata vijana wetu katika kuhifadhi na kuzipatia ufumbuzi, kwa lengo la kuboresha mradi wa kuhifadhi Qur’ani tukufu na kuweka mazingira mazuri kwao, kutokana na umuhimu wa pekee wa mradi huu.

Shughuli za kongamano baada ya makaribisho na kutoa shukrani kwa kazi kubwa wanayofanya ya kufuatilia watoto wao katika kuhifadhi na kuwahimiza kuendelea na jambo hilo takatifu, ukatajwa mkakati wa kila mwezi katika kuhifadhisha Qur’ani tukufu, na kujadili changamoto za wazazi wa wanafunzi wa tahfiidh (hususan wakati wa msimu wa masomo ya sekula).

Hali kadhalika zikajadiliwa sababu za kisaikolojia na kielimu zinazo weza kumsaidia mwanafunzi kuhifadhi, sambamba na kujaza dodoso maalum la wazazi, lililokua na mambo mbalimbali yanayohusu kongamano, kisha wazazi ambao watoto wao wamehifadhi Qur’ani nzima wakapewa zawadi.

Kumbuka kuwa kamati ya wataalamu iliyoundwa na Maahadi inalengo la kuboresha mradi wa kuhifadhisha Qur’ani tukufu, miongoni mwa watu waliopo kwenye kamati hiyo ni: Dokta Ni’matul-Asadi -mtaalamu wa mbinu za ufundishaji-, Muhandi Almayali -mkuu wa Maahadi na rais wa kamati-, Dokta Amiirah Aljuufi -mtaalamu wa seikolojia ya malezi ya kiislamu-.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: