Kutoa mihadhara ya elimu ya nafsi kwa wanafunzi wa Maahadi ya wahadhiri wa Husseiniyya

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya semina za elimu ya nafsi kwa wanafunzi wa Maahadi ya wahadhiri wa Husseiniyya, kwa kushirikiana na kituo cha utamaduni wa familia kilicho andaa ratiba ya semina hizi na mihadhara yake, itafanywa kila wiki ndani ya kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s).

Kwa mujibu wa maelezo ya makamo kiongozi wa idara hiyo bibi Taghridi Tamimi amesema: “Semina hizi zinafanywa kutokana na umuhimu wa somo la saikolojia, kwani ndio mlango wa kumtambua mwanaadamu na fikra zake, utambuzi huo unasaidia kufanya marekebisho na maendeleo, huwa na matokeo chanya katika maendeleo ya mwanafunzi, huongeza kiwango cha uwelewa, mihadhara hii ni sehemu ya mkakati wa Maahadi na inakamilisha selebasi yake”.

Akaongeza kuwa: “Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeandaa wahadhiri waliobobea katika fani hiyo, wameeleza kwa kina swala hilo sambamba na kueleza hatua na siri za mafanikio, pamoja na mambo mengi muhimu”.

Kumbuka kuwa mihadhara hii itafanywa kila wiki kwa kufuata ratiba maalum, nayo ni sehemu ya mkakati wa Maahadi wa kuboresha viwango vya wanafunzi wake, na kuwafanya kuwa vizuri katika kila jambo la kumjenga mwanafunzi mhadhiri wa Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: