Harakati za Qur’ani zinashuhudiwa katika Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, linafanya harakati mbalimbali za Qur’ani kwa wanawake, ambazo ni sehemu ya mkakati wa kueneza utamaduni wa Qur’ani kwa wanawake, na kuingiza katika nafsi zao na mienendo yao, kwa ajili ya kuandaa kizazi cha wanawake wasomi wa Qur’ani hapa mkoani.

Kiongozi wa tawi hilo, bibi Thamaru Kamalu-Dini ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kipindi hiki kimeshuhudia harakati tofauti za Qur’ani, ikiwemo hafla ya kuhitimu wanafunzi wa semina za majira ya kiangazi, jumla wa wanafunzi (200) wameshiriki kwenye semina hizo kutoka maeneo mbalimbali, na wanafunzi (60) wamepata ufaulu wa juu”.

Akaongeza kuwa: “Maahadi imefanya majaribio kwa wanafunzi wake wanaoshiriki kwenye semina za Qur’ani endelevu, kwa ajili ya kuangalia viwango vyao na uwelewa wao katika mada walizo soma, jaribio hilo limelenga kundi la wanaohifadhi Qur’ani tukufu, chini ya usimamizi wa jopo la maustadhat waliobobea katika somo la tahfiidh, hali kadhalika kulikua na mitihani ya wanafunzi walioshiriki kwenye semina za usomaji sahihi kwa kufuata hukumu za usomaji wa Qur’ani”.

Akamaliza kwa kusema: “Miongoni mwa shughuli ambazo Maahadi imekua ikizifanya ni majlisi na mahafali za usomaji wa Qur’ani, ilifanya majlisi ya usomaji wa Qur’ani iliyo husisha kundi la wakinadada wasomi wa Qur’ani katika Maahadi, na thawabu za usomaji huo zikaelekezwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani, linalenga kusambaza elimu ya Dini kwa wanawake, ikiongozwa na “elimu ya Qur’ani”, na kuchangia kuandaa kizazi cha wanawake wasomi wa Qur’ani, wenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika sekta zote za Qur’ani tukufu na fani zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: