Atabatu Abbasiyya tukufu yafunya ufunguzi wa shule mbili za msingi ya wavulana na wasichana katika mji wa Baabil

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Jumatano mwezi (26 Rabiul-Awwal 1443h) sawa na tarehe (2 Novemba 2021m) imefungua shule mbili za msingi ya wavulana na wasichana katika mkoa wa Baabil, ufunguzi huo umeongozwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na makamo wake pamoja na baadhi ya viongozi.

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi amesema: “Leo tumefungua mradi wa shule mbili za msingi, ya wavulana na wasichana katika mkoa wa Baabil, kila shule inadarasa (15) pamoja na maabara na uwanja wa katikati wa bustani”.

Akaongeza: “Atabatu Abbasiyya tukufu imekua ikifanya kila iwezalo kuboresha hali ya elimu nchini, kuanzia shule za awali hadi vyuo vikuu, matokea ya taasisi za elimu zilizo chini yake yamethibitisha hilo, kufuatia matokeo mazuri ya wanafunzi wake, tumependa kuleta uzowefu wetu katika mkoa wa Baabil katika kuhudumia wakazi wake”.

Akaendelea kusema: “Karibu miaka miwili kitengo cha majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimekua kikijenga majengo ya miradi mbalimbali ya Ataba tukufu, daima tumekua tunakamilisha miradi ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora mkubwa”.

Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Rashidi Mussawi amesema: “Baada ya shule za Al-Ameed kuchukua nafasi kubwa katika mji wa Karbala, leo tumeingia katika mkoa wa Baabil, kutokana na umuhimu wa mji huu mtukufu ambao uliwahi kuwa kitovu cha elimu na wanachuoni”.

Akaongeza kuwa: “Miaka ya hivi karibuni mkoa umepitia hali ngumu iliyoathiri sekta ya malezi na elimu, leo tumekuja kuendeleza sekta hiyo kwa wakazi wa mji huu kama tunavyo fanya katika mkoa wa Karbala”.

Tambua kuwa shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zinafaulisha vizuri kila mwaka, na zinamikakati ya kuboresha walimu wake sambamba na kutumia njia za kisasa katika ufundishaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: