Wataalamu wa Alkafeel wa mafunzo ya uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza wanaomboleza kifo cha shahidi wao

Maoni katika picha
Wataalamu wa Alkafeel wa mafunzo ya uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza chini ya kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Jumatano, wameomboleza kifo cha muokozi na mkufunzi wa kimataifa Muhammad Raadhi Qassim.

Rais wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu dokta Muhammad Hassan Jaabir amesema: “Leo ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, tumeomboleza kifo cha muokozi aliyefanya kazi kubwa ya kulinda maeneo matakatifu chini ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, na mjumbe wa wataalam wa mafunzo ya uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza, alikufa kishahidi akiwa anatekeleza wajibu wake katika mji wa Qaaimu”, akasema kuwa: “Bendera ya jihadi, utumishi, Abulfadhil Abbasi (a.s) na bendera ya taifa, zote ni sawa na bendera moja, tunafanya kazi kwa ajili ya kupandisha bendera hizo na kulinda damu za wananchi chini ya bendera hizo, ujumbe huu tunapenda kuuwasilisha”.

Familia ya shahidi imeshukuru na kuipongeza Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia wataalam wa Alkafeel, kwa kumkumbuka mtoto wao shahidi, wakasema jambo hilo sio geni kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwani imekua mstari wa mbele kufuatilia mateka, kutembelea familia za mashahidi na kutembelea majeruhi walioitikia wito wa fatwa tukufu ya kujilinda.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: