Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya yafanya shindano la (Usomaji wa Qur’ani) awamu ya tano

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya inaendesha shindano la (usomaji wa Qur’ani) awamu ya tano, wameshiriki zaidi wa wasomaji (40).

Shindano limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na bwana Ali Haadi, ukafuata utaratibu wa shindano uliokua na hatua mbili, hatua ya kwanza imeshuhudia ushindani mkubwa, hapo ukafanyika mchujo na kupata wasomaji (10) walio ingia hatua ya pili, baada ya kumalizika hatua hiyo yakatangazwa majina ya washindi na wakapewa zawadi.

Tambua kuwa shindano hili lilikua rasmi kwa ajili ya wasomaji wa tawi la Hindiyya, na limefanywa chini ya kamati ya majaji mahiri, lengo la shindano hili ni kuwajengea uwezo na kuwaendeleza wasomaji ili kuwaanda waweze kushiriki kwenye mashindano makubwa ya kitaifa na kimataifa.

Inapendeza kusema kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kusambaza elimu ya Qur’ani na kuchangia katika kuandaa jamii yenye uwelewa mzuri wa Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: