Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Khairul-Juud, chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, linashiriki katika maonyesho ya kilimo na mazao ya wanyama yanayo fanyika Arbiili, kwa lengo ya kusaidia uzalishaji wa taifa na shughuli za kilimo kwenye mikoa tofauti hapa nchini.
Mhandisi Falahu Fatla mkuu wa masoko na mauzo katika shirika hilo amesema: “Katika maonyesho haya tuna mbolea isiyo na kemekali na inafanya vizuri katika kilimo hapa nchini, pamoja na bidhaa zingine nyingi zinazo kidhi mahitaji ya soko la ndani”.
Akaongeza kuwa: “Shirika linafanya kazi ya kuboresha sekta ya kilimo kwenye mikoa tofauti ya Iraq, na kuongeza kiwango cha uzalishaji wa taifa”.
Akabainisha kuwa: “Shirika limejipanga kufikisha bidhaa zake kwenye mikoa yote, kwa lengo la kuboresha sekta ya kilimo, na kuhakikisha watu wananufaika na bidhaa hizi muhimu”.
Akasisitiza kuwa: “Bidhaa zinazotengenezwa na shirika la Khairul-Juud zinaubora wa hali ya juu na salama kwa mazingira”, akasema: “Bidhaa hizi hazina athari mbaya katika mazingira wala kwenye ardhi”.
Akaendelea kusema kuwa: “Udongo wa Iraq unachangamoto nyingi, chamgamoto ya chunvi, mfinyanzi na zinginezo, jambo ambalo linamuhitaji mkulima kutumia mbolea maalum, inayoweza kupambana na changamoto hizo na kuongeza uzalishaji, na jambo hilo ndio linalofanywa na shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Khairul-Juud”.