Wito wa kushiriki katika nadwa kuhusu Shekh Kaf’ami

Maoni katika picha
Idara ya kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inatoa wito kwa wadau wote wa utamaduni na turathi wa kushiriki kwenye nadwa isemayo (Shekh Kaf’ami aliyefariki mwaka wa -905h- Maisha yake na juhudi zake kielimu), siku ya Ijumaa tarehe (12 Novemba 2021h) saa tatu asubuhi ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Nadwa ni sehemu ya harakati za kituo na maandalizi ya kongamano la kielimu na kimataifa awamu ya pili, liitwalo: (Harakati za Karbala kielimu katika karne ya kumi hijiriyya), litakalo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Turathi zetu utambulisho wetu) tarehe (17 – 18 Novemba 2022) sawa na mwezi (23 – 24 Rabiul-Aakhar 1444h).

Nayo ni moja ya mfululizo wa nadwa zinazofanywa na kituo, zinazo husu kuwakumbuka watu muhimu katika mkoa wa Karbala, waliofanya harakati za kielimu katika mji huu, nadwa hizo huwa na mada tofauti.

Unaweza kushiriki nadwa tajwa kupitia jukwaa la (ZOOM) kwa link ifuatayo:

https://us02web.zoom.us/j/7820585457?pwd=TkZLeU1MY2d5eUpqeTJ5WUJTRHlVUT09

Meeting ID: 782 058 5457
Passcode: 1
Idara ya kituo cha turathi za Karbala itatoa vyeti vya ushiriki kwa watu wote watakao shiriki nadwa hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: