Chakula mbalimbali kinaonyeshwa katika shirika la Nurul-Kafeel kwenye maonyesho ya Arbiil

Maoni katika picha
Shirika la Nurul-Kafeel linazalisha chakula na bidhaa za wanyama (ni moja ya mashirika ya Atabatu Abbasiyya tukufu), linashiriki katika maonyesho ya mazao na bidhaa za wanyama yanayo fanyika Arbiil chini ya wizara ya kilimo na kauli mbiu isemayo: (Kwa Pamoja tunasaidia uzalishaji wa taifa na kuimarisha upatikanaji wa chakula).

Mkuu wa shirika Ustadh Jafari Hussein Alqutbu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ushiriki wetu katika maonyesho haya, ambayo kuna zaidi ya mashirika (50) tofauti kutoka mikoa mbalimbali ya Iraq, ni fursa ya kufungua uwanja wa mawasiliano na ushirikiano baina ya mashirika, na kwa upande mwingine pamoja na watumiaji wa bidhaa zetu, sambamba na kutambulisha bidhaa tunazotengeneza ambazo zinahitajiwa na familia za wairaq”.

Akaongeza kuwa: “Bidhaa zetu zinatokana na malighafi za ndani na zinaubora mkubwa, zimekidhi vigezo vya ubora kimataifa, pamoja na kukubalika kwake sokoni kutokana na udogo wa bei yake, tawi limefanya kazi ya kutambulisha shirika na bidhaa zake”.

Akabainisha kuwa: “Tawi limeonyesha aina mbalimbali za chakula, kama vile nyama nyekundu na nyeupe, na namna zinavyo andaliwa pamoja na aina tofauti za vyakula, limepata muitikio mkubwa, hii sio mara ya kwanza kushiriki kwenye maonyesho, tumesha shiriki mara nyingi kwenye maonyesho ya kitaifa na kimataifa, ambako tumefanya vizuri na kuwa chachu ya kuendelea kushiriki kwenye maonyesho mengine”.

Tawi letu limetembelewa na asilimia kubwa ya watu wanaokuja kwenye maonyesho haya, pamoja na vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa, wote wamefurahishwa na kupongeza bidhaa walizoona, na kuomba kuanzisha ushirikiano wa kibiashara zaidi, ili waweze kunufaika na bidhaa hizi zinazo kidhi mahitaji yao, ukizingatia kuwa bidhaa zetu ziko sawa au zinashinda ubora wa bidhaa zinazo toka nje ya nchi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: